Quick Tv Africa Swahili

MTU MASHUHURI: QCHIEF AWAOMBA RADHI MASHABIKI BAADA YA KUTOA LUGHA YA MATUSI KWA DIAMOND PLATNUMZ NA SALLAM SK

Dar es Salaam. Abubakar Katwila maarufu QChief @official_qchief amewaomba radhi mashabiki na wadau wa muziki nchini Tanzania kwa kutoa lugha chafu dhidi ya msanii mwenzake Nassib Abdul @diamondplatnumz na meneja wa mkali huyo wa wimbo wa Waah  Sallam Sharaf alimaarufu kama @sallam_sk

Alilalamika kuwa licha ya picha yake kuonekana hakuwa akilifahamu tamasha hilo na wala hakualikwa.

Msanii huyo aliyetamba zaidi mwanzoni mwa miaka ya 2000 amesema alichukizwa na jambo hilo na hasira ndio zilimfanya kutoa lugha chafu.

Mimi sina ubaya ni binadamu wa kawaida kwa hiyo nakasirika, nachukia na naumia mtu anaponifanyia mambo ambayo siyapendi.” Q chilla ameendelea kwa kusema.

Tuliwaandikia barua ya kisheria na wameijibu juzi lakini nisingependa kusema wametujibu nini kwa sababu ni suala lililopo mikononi mwa vyombo vya dola kwa sasa,” amesema hivyo akiongea na vyombo vya habari

Hatua hiyo imekuja Mara baada ya Q chilla kuposti katika ukurasa wake @official_qchief tarehe moja January kuwa @official_qchief

Habari watanzania na industry yote ya mziki kwa ujumla.i think I need to address this issue to @diamondplatnumz @hellenkazimoto@sallam_sk na uongozi mzima wa @wcb_wasafi@tigo_tanzania nimepokea simu nyingi sana Jana mpaka today kuwa mbona sikuonekana kwenye show.

As you all know mziki mimi ndo unanilisha na kuendesha mimi na familia yangu na pia niko na watu nyuma yangu (management) ambao wameniona mtu wa Ajabu sana.

Kwani jina langu limeonekana kwenye poster ya  na nilikuwa kama one of the performer siku ya tarehe 30/Jan #uwanjawauhuru kitu ambacho sio kweli kwani sio mimi wala management ilizungumza na uongozi wa  kuhusu show hiyo.nimejaribu kuwapigia lakini wanaleta sababu kwamba watu wamechoka kwasababu ya show.hivo basi management yangu na mimi tumetoa siku ya leo kuwa ya mwisho kupata maelezo juu ya utapeli huu kutumia jina langu kupata fans wangu na wao kujiongezea credibility.

Naomba mu act haraka on this kwani tutakuja laumiana.sitaki matatizo na mtu napambana on my own naomba muwaeleze watanzania either video or mahandishi.alafu hatua nyingine zitafata.Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.Asubuhi njema.

Pamoja na video zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Q Chief akionekana kutoa lugha chafu dhidi ya wawili hao akiwatuhumu kutumia picha yake kwenye bango linaloonyesha orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye shoo ya Wasafi Tumewasha iliyofanyika jijini Dar es Salaam Januari 30, 2021

Comments

0 comments

Related posts

Waziri Dorothy Gwajima amemu ahidi Makamu raisi wa Tanzania mh.

Quick Tv Africa

IJUE TANZANIA DINI ZAO , UTAMADUNI, MALIASILI NA VITU WANAVYO VIPENDA

Quick Tv Africa

MTU MASHUHURI : DIAMOND PLATINUM ATOA AHADI HII KWA SAMIA SULUHU MAKAMU WA RAISI TANZANIA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Quick Tv Africa