Breaking News Quick Tv Africa Swahili

IJUE TANZANIA DINI ZAO , UTAMADUNI, MALIASILI NA VITU WANAVYO VIPENDA

Tanzania ipo mashariki mwa bara la Afrika huku likiwa limezungukwa na nchi mbalimbali
Upande wa kaskazini imepakana na Kenya na Uganda , huku maghalibi ikiwa imepakana na nchi ya Rwanda , Burundi na jamuhuli ya demokrasia ya Kongo, pia upande wa kusini imepakana na nchi ya Zambia, Malawi, na msumbiji wakati upande wa mashariki kuna bahari ya Hindi

JINA TANZANIA
Tanzania ni nchi yenye amani na upendo jina hili limetokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar baada ya waasisi na wapigania Uhuru Mwalimu Julius kambarage Nyerere (kiongozi mkuu wa TANU) kutoka Tanganyika pamoja na Abeid Amani Karume (kiongozi mkuu wa chama cha ASP) kutoka Zanzibar ndio walio unganisha nchi hizi na kufanya kuwa nchi moja ya Jamuhuli ya muungano wa Tanzania tarehe 26 April 1964

LUGHA YA TANZANIA

kiswahili ndiyo lugha ya taifa la Tanzania iliyopitishwa na awamu ya kwanza ya uongozi ambayo ni ya Mwalimu nyerere na alikuwa mtu ambaye anahamasisha sana watu watumie kiswahili na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa maana hadi leo Watanzania wanatunatumia lugha hii kuwasiliana licha ya kuwepo na makabira zaidi ya 125 lakini kwa kutumia kiswahili kunafanya mtanzania yeyote kuenda sehemu yoyote na kuweza kuelewana

VITU WANAVYO ABUDU

Watanzania wanaabudu katika mapango, milimani pia katika miti mikubwa kama mbuyu lakini baada ya kuja wamisionali na wakoloni Ukristo na Uislamu ndiyo dini kuu ila hii haimaanishi watu wameacha kuabudu kwenye mapango ,miti na kwenye milima kwani vijijini bado wanaendeleza utamaduni huo wakiongozwa na machifu wao
Pamoja na kuwa kila mtu anaamini dini yake hii haifanyi watanzania kuacha kupendana kutokana na Mwalimu nyerere kusisitiza Sera ya ujamaa na lugha ya kiswahili vitu hivi vimechangia watanzania kuwa wamoja na kushirikiana mambo mbalimbali bila kujali kabira wala dini na kuzidi kufanya Tanzania kuwa ya amani ni kawaida mtanzania akifika kazini au dukani kusalimia pia kuitana “Dada” na “kaka” tofauti na nchi zingine

UTAMADUNI MAVAZI WANAYOPENDA

Watanzania wengi wanapenda kuvaa kanga hizi ni aina ya kitambaa cha pamba linalo valiwa na wanawake asili yake ni kutoka Zanzibar katika karne ya 19 ni nyepesi yenye rangirangi na inakuwa na maandishi ambayo ni methali au misemo mbalimbali,
Pia wanapenda kuvaa vitenge hili ni vazi ambalo lipo kama kanga ila tofauti yake yenyewe ni nzito na zina michoro mbalimbali kama maua, wanyama namengineyo

VYAKULA WANAVYOPENDA

Watanzania wanapenda kula wali, ugari, kande na viazi . ila wali unapendwa sana hasa ukiwa na maharagwe hapo ndiyo utaona hata watoto wakitanzania kikipikwa chakula hicho hawasinzii hadi watakavyokula
Watanzania wanapenda kula nyama wanapenda kula wanyama pori kama nyati, swala , digi digi nazinginezo na kuna makabila wanayojihusisha na uwindaji mfano wamang’ati, wasandawe pia wamasai vilevile kuna wafugaji ambao ni wasukuma na wengineo hii inafanya Watanzania kula sana nyama za ng’ombe na mifugo mingine mtu mmoja mmoja sana utakuta hali nyama kabisa

MALIASILI ZA TANZANIA

Tanzania inavivutio vingi kama vile milima mbalimbali mfano mlima Kilimanjaro huu ni mlima mkubwa kuliko yote Afrika pia kuna milima mingine kama milima ya usambara, milima ya Udzungwa

Vilevile Kuna mbuga mbalimbali za wanyama kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro na Manyara

pia kuna maporomoko ya mto Ruaha na mengineyo

SANAA

Kwa Tanzania kuna sanaa ya Kucheza, kuigiza, uchoraji, na vimeenea kwa uchoraji wa tingatinga pia vinyago vya wamakonde vinapendwa sana
Lakini sanaa iliyokuwa zaidi Tanzania ni muziki, Ngoma ndiyo inayoongoza kwenye muziki wa Tanzania kwani kila kabila lina ngoma zao mfano mang’oma kutoka kabila la Wanyakyusa.

muziki wa bongo flava ndiyo uliokuwa zaidi Tanzania ukiwa na wasanii wakubwa ambao wanajulikana karibu na dunia nzima kama Msanii Diamond platinums, vannesa mdee, rayvanny, harmonize, zuchu na wengineo huu ni mziki ambao umetokana na hip pop, R & B na kwasasa Nigeria bongo flava ni mziki ambao una radha ya kipekee na ninzuri na sasa umekuja mziki mpya unaoitwa singeli hii ni aina ya mziki ambao ni maarufu sana katika maeneo yanayo kaliwa na waswahili au watu wa pwani singeli huchukuliwa kama mnanda au mchiriku wa kisasa na umetokana na muunganiko wa muziki wa Taarabu, bongo flava, mchiriku na vanga(mdundiko) la kizaramo ndilo limezaa mziki huo
Vilevile mziki wa taarabu ambao unapendawa na watu wa pwani na maeneo mengine ambayo asili yaki ni Zanzibar inamchanganyiko wa midundo ya kiarabu na ngoma za pwani.

Comments

0 comments

Related posts

MEET THE GIRL THAT FEELS NO PHYSICAL PAIN

Ayomide Damzy

NIGER: Heavily armed attackers stormed Gaigorou on Saturday

Quick Tv Africa

TECHNOLOGY: China and Russia revelled plan to build lunar space station

Quick Tv Africa

Leave a Comment